Saturday, May 25, 2013

MAZZARRI KOCHA MPYA INTER MILAN.

KLABU ya Inter Milan ya Italia, imemteua kocha wa zamani wa Napoli Walter Mazzarri kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kumtimua Andrea Stramaccioni kufuatia matokeo mabaya ya msimu uliopita yaliyopelekea klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Serie A. Inter ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka 2010 wamekuwa katika matatizo makubwa na kubadilisha makocha zaidi ya watano toka Jose Mourinho alipoondoka. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo walimshukuru Stramaccioni kwa kazi na weledi mkubwa alioonyesha katika msimu huo mgumu na kuthibitisha kuingia mkataba wa miaka miwili na Mazzarri. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa aliyekuwa kocha wa muda wa Chelsea Rafael Bernitez atajiunga na Napoli kuziba nafasi ya Mazzarri wakati kocha wa AC Milan Massimiliano Allegri ataendelea na kibarua chake.

No comments:

Post a Comment