Sunday, May 12, 2013

MILAN WATAKOSEA WAKIMTIMUA ALLEGRI - AMBROSINI.

KIUNGO nyota wa kimataifa wa Italia na klabu ya AC Milan, Massimo Ambrosini ameshauri kuwa haitakuwa vyema kama klabu hiyo ikiamua kukatisha mkataba na kocha wake Massimiliano Allegri mwishoni mwa msimu huu. Kumekuwa na maswali yasiyokuwa na majibu kuhusu mustakabali wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 kuendelea kuinoa klabu hiyo baada ya msimu kumalizika, lakini Ambrosini anaamini kuwa Allegri anastahili kuendelea kuwepo hapo kwa nzuri anayoifanya katika misimu michache iliyopita. Ambrosini amesema Allegri amefanya vyema na kutulia katika kipindi kigumu walichopitia na pia ameweza kuwatuliza wachezaji hivyo utakuwa ni uamuzi mgumu kumuondoa kocha mbaye ameipa mafanikio muhimu klabu hiyo.Kiungo huyo aliendelea kusema kuwa anafikiri wakati umefika Milan wakumthibitisha kwamba kocha huyo ataendelea kuwepo hapo msimu ujaolakini hilo litategemea na nini rais anataka. Allegri alianza kuinoa Milan katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2010 na toka achukue mikoba hiyo ameingoza klabu hiyo kunyakuwa taji moja la Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Serie A.

No comments:

Post a Comment