Wednesday, May 15, 2013

SAO PAULO INAWEZA KUPOTEZA HAKI ZA KUANDAA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA - FIFA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeonya maofisa wa jiji la Sao Paulo kwamba wanaweza kupoteza haki ya kuandaa baadhi ya mechi za Kombe la Dunia 2014 kwasababu ya kuchelewa kukamilika kwa uwanja. Tishio hilo limeleta hasira kwa wamiliki wa kiwanja cha Corinthians ambao wamedai kuwa FIFA wanaweza kuwanyima haki hiyo kama wakitaka lakini hawawezi kufanya kazi chini shinikizo. Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema shirikisho hilo haliwezi kukubali kitu chochote ambacho kitapelekea uwanja huo ambao utachezwa mechi sita ikiwemo ile ya ufunguzi, kushindwa kufikia tarehe ya mwisho waliyowekewa. Mafundi tayari wameonya kuwa uwanja huo hautarajiwa kuwa tayari mpaka mwishoni mwa Februari mwakani. Valcke amesema kuanzia sasa mpaka hapo tiketi zitakapoanza kuuzwa wana uwezo wa kubadilisha mechi hizo katika viwanja vingine vilivyo tayari, hivyo wanasubiri mpaka Agosti mosi ili kuangalia uwezekano wa kubadilisha viwanja.

No comments:

Post a Comment