Wednesday, May 15, 2013

SCOLARI AKINGIA KIFUA UTEUZI WA NEYMAR.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe Scolari amemkingia kifua Neymar kufuatia tuhuma za mshambuliaji huyo kushuka kiwango katika klabu klabu yake kwa miezi ya karibuni. Nyota huyo anayecheza klabu ya Santos ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa katika kikosi kitakachoshiriki Kombe la Shirikisho mwezi ujao na kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 amedai kuwa kiwango chake ndicho kilichopelekea kumuita katika kikosi chake. Scolari amesema Neymar amekuwa akicheza vyema katika ngazi ya klabu ingawa wengi hawatakubaliana name kwenye hilo lakini kwa maono yetu ya kiufundi hatuoni tatizo lolote kuwa naye kwenye kikosi. Scolari pia alitetea uamuzi wake wa kuwaacha nyota wengine wakongwe kama Ronaldinho na Kaka akidai kuwa bado wana nafasi ya kuwemo katika kikosi katika siku zijazo kama wataimarisha viwango vyao kuliko ilivyo hivi sasa. 

No comments:

Post a Comment