KLABU ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa mara nyingine itacheza mechi zake za Europa League msimu ujao mbali na uwanja wao wa nyumbani baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka barani-UEFA humo kwasababu za kiusalama. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao wake imedai kuwa baada ya kufanya utafiti wa usalama katika mji wa Kaskazini wa Caucasus ambao klabu hiyo inatoka wamegundua kuwepo usalama mdogo hivyo hawatoruhusu timu hiyo kucheza mechi zake nyumbani. UEFA imeitaka klabu hiyo kutafuta uwanja mbadala kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za Europa League msimu wa 2013-2014. Anzhi walimaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Urusi msimu uliopita na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment