Thursday, June 20, 2013

SERENA AOMBA RADHI.

MWANADADA nyota wa mchezo wa tenisi anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa uapnde wanawake, Serena Williams ameomba radhi kwa aliyoitoa katika gazeti la Rolling Stone kuhusiana na kesi ya ubakaji. Nyota huyo ambaye anatarajiwa kutetea ubingwa wake wa michuano ya Wimbledon alikaririwa na gezeti kuhusiana na kesi hiyo inayoendelea katika mji wa Steubenville, Ohio, Marekani. Katika kesi hiyo wachezaji wawili wa mpira wa miguu wa kimarekani wanatuhumiwa kumbaka msichana aliyelewa mwenye umri wa miaka 16 tukio ambalo walilifanya Machi mwaka huu. Gazeti hilo la Rolling Stone lilimkariri Williams akidai kuwa hamlaumu msichana huyo lakini kama una umri wa miaka 16 na unakunywa kiasi hicho wazazi wako wanatakiwa kukufundisha kwamba usipokee kinywaji kutoka kwa mtu usiyemfahamu.Kauli yake hilo ilishambuliwa na watu mbalimbali nchini humo mpaka kupelekea nyota kuomba radhi akidai kuwa hakumaanisha kama watu wanavyofikiri.

No comments:

Post a Comment