Thursday, June 20, 2013

DROGBA APORWA.

GAZETI moja la kila wiki nchini Ivory Coast limechapisha taarifa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Didier Drogba ameporwa wakati akiwa likizo katika hoteli moja nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa mshambuliaji huyo anayekipiga katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki aligundua kuwa ameporwa fedha zake kiasi cha euro 7,500 alizokuwa amehifadhi katika beki lake wakati aliporejea kwenye chumba chake alichokuwa amepanga katika ghorofa ya 11 kwenye hoteli hiyo. Mara baada ya kugundua kuibiwa nyota huyo aliufahamisha uongozi wa hoteli hiyo ya nyota tano ambao nao walipiga simu polisi lakini juhudi zao hazikufanikiwa kuzipata fedha hizo. Hiyo sio mara ya kwanza kwa nyota wa soka nchini humo kuibiwa fedha au vito vya vya thamani wakati wakiwa likizo kwani beki wa kushoto wa nchi hiyo anayekipiga katika klabu ya Stuggart ya Ujerumani Boka Arthur naye alikumbwa na tukio kama hilo kwenye hoteli hiyohiyo.

No comments:

Post a Comment