BENFICA YAMUONGEZA MKATABA JESUS.
KLABU ya Benfica ya Ureno imetangaza kumuongeza mkataba mpya kocha wake Jorge Jesus mpaka katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2015. Kulikuwa na wasiwasi kama kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 anaweza kubakia katika klabu hiyo baada ya kumaliza msimu na kuambulia patupu. Hata hivyo Jesus sasa amemaliza utata huo kwa kusaini miaka miwili zaidi na klabu hiyo inayotoka katika jijini Lisbon. Jesus alianza kuinoa Benfica kuanzia mwaka 2009 na kuingoza kushinda taji moja la Ligi Kuu na matatu ya Kombe la Ligi la nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment