Wednesday, June 5, 2013

LEWANDOWSKI ANA UHAKIKA WA KUONDOKA DORTMUND.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Roberto Lewandowski ana uhakika kuwa klabu hiyo itamuachia aondoke katika kipindi cha majira ya kiangazi hivyo kuiongezea nguvu klabu ya Bayern Munich ambayo inataka kumsajili. Dortmund wamekuwa wakikataa ofa mbalimbali wanazopata kwa timu zinazomhitaji nyota huyo lakini mwenyewe ameonyesha kutokuwa na wasiwasi wa kuondoka klabuni hapo katika kipindi hiki. Akihojiwa nyota huyo amesema anategemea mambo ya kwenda sawa kwa kila upande na yeye aende kucheza katika klabu ya ndoto zake. Nyota huyo mwenye miaka 24 ambaye mkataba wake na Dortmund unamalizika 2014, amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali vikubwa huku Bayern wakiongoza na kufuatia na Manchester United ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment