Wednesday, June 5, 2013

MERTINEZ MENEJA MPYA EVERTON.

MENEJA wa zamani wa klabu ya Wigan Athletic, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Everton akichukua nafasi ya David Moyes aliyekwenda Manchester United. Martinez mwenye umri wa miaka 39 alifanikiwa kutwaa taji la Kombe la FA msimu huu, lakini aliomba kuondoka baada ya kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kubakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Mwenyekiti wa Wigan, Dave Whelan alimruhusu kocha huyo raia wa Hispania kuondoka na tayari wako katika mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa kuziba pengo hilo. Martinez ambaye pia amewahi kuinoa Swansea City alijiunga na Wigan Juni mwaka 2009 na Aston Villa walitaka kumchukua mwaka 2011 lakini aliamua kubakia Wigan mpaka msimu huu alipoamua kuelekea Everton.

No comments:

Post a Comment