Wednesday, June 5, 2013

SNEIJDER AKIRI KUWASILIANA NA MOURINHO.

KIUNGO wa klabu ya Galatasaray, Wesley Sneijder amekiri kuwa bado anawasiliana na Jose Mourinho toka kocha huyo mpya wa Chelsea aondoke katika klabu ya Inter Milan kwenda Real Madrid na kuongeza tetesi kuwa atajiunga na kocha huyo Stamford Bridge. Sneijder ambaye amejiunga Galatasaray katika kipindi dirisha dogo la usajili la Januari, akihojiwa alishindwa kukataa kabisa uwezekano wa kuelekea Chelsea katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Kiungo amedai kuwa amekuwa na mahusiano mazuri na Mourinho toka akiwa Inter na mpaka sasa na alipoulizwa kama ataenda Chelsea kuungana nae, nyota huyo alijibu kuwa katika soka soka huwezi kujua kitu kitakachotokea mbele lakini anafuraha katika klabu yake ya sasa. Sneijder mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akipondwa na baadhi ya wadau wa soka nchini Uturuki kwa kucheza chini ya kiwango ingawa mwenyewe alijitetea kwa kudai kuwa hakuna mchezaji anayeweza kucheza katika kiwango cha juu katika maisha yake yote ya soka.

No comments:

Post a Comment