Wednesday, June 5, 2013
NEYMAR ATAMZIDI MESSI - PELE.
NGULI wa soka wa Brazil, Pele anaamini kuwa mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na Barcelona, Neymar ana nafasi ya kukomaa na kuwa bora kuliko Lionel Messi. Nyota huyo wa zamani wa Santos alikamilisha uhamisho wake kwenda La Liga uliogharimu kiasi cha euro milioni 57 Jumatatu iliyopita kabla ya kutambulishwa mbele ya mashabiki wapatao 56,000 waliofurika katika Uwanja wa Camp Nou. Akihojiwa katika utambulisho wake, Neymar alibainisha ni gani anavyotazamia kumsaidia Messi ili aendelee kung’ara zaidi duniani ingawa hata hivyo Pele anatarajia kuwa nyota huyo atamzidi Messi. Pele amesema kwa miaka miwili iliyopita kiwango cha Neymar kimekuwa, ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili vizuri na mzuri kwenye mipira ya vichwa ndio maana huwa anasema nyota huyo ana uwezo kuwa bora zaidi ya Messi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment