RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amesema Zinedine Zidane ana vigezo vyote vinavyohitajika kuchukua nafasi ya Jose Mourinho lakini anadhani bado anahitaji uzoefu zaidi kabla ta kukabidhiwa mikoba hiyo. Perez amesema Zidane ana kila kitu ambacho kocha anatakiwa kuwa nacho na kazi hiyo anaiweza lakini bado anahitaji uzoefu ili kukabidhiwa majukumu makubwa kama hayo. Kwasasa chaguo la kwanza la Madrid katika kutafuta mbadala wa Mourinho ni kocha wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti ingawa Perez alishindwa kuliongelea kwa kuogopa kuwachukiza PSG ambao bado wamemng’ang’ania kocha huyo. Zidane ambaye ameichezea Madrid kuanzia mwaka 2001 mpaka 2006 kwasasa ni mkurugenzi wa michezo na kocha wa vijana wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment