Monday, June 24, 2013
CAMACHO CHALI CHINA.
CHAMA cha Soka nchini China-CFA kimetimua koha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Jose Antonio Camacho baada ya kuinoa timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili. Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na Hispania ametimuliwa baada ya nchi hiyo kushindwa kufanya vyema katika mechi tatu za kirafiki walizocheza Juni mwaka huu kikiwemo kipigo cha aibu cha mabao 5-1 kutoka kwa Thailand na kutolewa mapema katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka jana. Katika taarifa iliyotolewa na CFA imedai kuwa wamefikia uamuzi huyo baada ya pande zote kukubaliana kuvunja mkataba na tayari taratibu za kumpata mbadala wa Camacho zimeshaanza. Camacho aliteuliwa Agosti mwaka 2011 na katika kipindi chote hicho nchi hiyo imechapwa mechi 11 kati ya 20 kikiwemo kipigo cha mabao 8-0 kutoka kwa Brazil Septemba mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment