Tuesday, June 4, 2013

ERIKSSON AIBUKIA CHINA.

KLABU ya Guangzhou R&F inayoshiriki Ligi Kuu nchini China, imemteua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Sven-Gran Eriksson kuwa kocha mpya wa klabu hiyo. Kwa mujibu a taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo Eriksson ambaye ambaye aliachia nafasi yake kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Al Nasr ya Muungano wa Falme za Kiarabu, amejiunga na Guanghzou kwa mkataba wa miezi 18. Uteuzi huo utamfanya Eriksson raia wa Sweden kukutana na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Marcello Lippi ambaye anawafundisha mabingwa wa sasa wa ligi hiyo Guangzhou Evergrande. Pamoja na klabu hiyo kutotoa kiasi atakacholipwa Eriksson lakini vyombo vya habari nchini Uingereza vimekisia kuwa kocha huyo atakuwa akipewa kiasi cha paundi milioni 2 kwa mwaka katika klabu hiyo ambayo imemaliza katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.

No comments:

Post a Comment