KIUNGO mpya wa klabu ya Manchester City, Jesus Navas amedai kuwa amefurahishwa na kumalizika kwa uhamisho wake kutoka klabu ya Sevilla na sasa ana hamu kubwa ya kuisaidia klabu hiyo katika mipango yao huko mbele. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alisaini mkataba wenye thamani ya euro milioni 20 kwenda Etihad baada ya kutumia muda mwingi wa soka katika La Liga. Navas amesema aliichagua kwenda City miezi minne iliyopita na sasa anajisikia ahueni baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho. Nyota huyo ataungana na Manuel Pellegrini ambaye muda wowote atatajwa kama kocha mpya wa klabu hiyo akichukua mikoba ya Roberto Mancini aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment