Wednesday, June 26, 2013
FENERBAHCE WAFUNGIWA MIAKA MIWILI KWA KUPANGA MATOKEO.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeifungia klabu ya Fenerbahce ya Uturuki kushiriki michuano ya bara hilo kwa misimu miwili huku pia klabu ya Besiktas nayo ikifungiwa msimu mmoja. Klabu hizo mbili zenye maskani yake jijini Istanbul zimekumbwa na dhahma hiyo baada ya kukutwa na hatia ya upangaji wa matokeo mwishoni mwa msimu wa 2010-2011. Katika taarifa ya UEFA iliyotolewa baada ya uchunguzi ilidai kuwa Fenerbahce wamefungiwa kwa misimu miwili kushiriki michuano hiyo kuanzia msimu unaokuja huku wakitakiwa kutofanya kosa kama hilo kwa kipindi cha miaka mitano watakaoyokuwa chini uchunguzi. Fenerbahce ambao walikuwa washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu unaokuja baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo sasa wataikosa michuano hiyo pamoja na msimu ujao kama wakifuzu tena kutokana na adhabu waliyopewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment