ALIYEKUWA kocha wa viungo wa timu ya taifa ya Argentina katika michuano ya Kombe la dunia 2010, Fernando Signorini ameonya kuwa Lionel Messi anahitajika apate mapumziko ili aweze kucheza michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani akiwa katika kiwango cjake cha juu. Nyota huyo wa Barcelona amekuwa akikumbwa na matatizo ya misuli katika miezi ya karibuni na Signorini anafikiri mshambuliaji huyo anahitaji mapumziko ya muda mrefu ili aweze kupina kikamilifu. Signorini amesema Messi anacheza zaidi ya mechi 100 kwa mwaka akiwa na Barcelona na timu yake ya taifa kitu ambacho kinamuweka katika hatari ya kutokuwa katika kiwango chake cha juu ifikapo michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Amesema haitawezekana kwa soka la kisasa mtu ucheze idadi hiyo ya mechi nab ado uendelee kucheza kwa kiwango cha juu hivyo la msingi ni nyota huyo kupewa likizo ndefu pamoja na mke na mtoto wake ili aweze kupona vizuri. Katika msimu wa mwaka 2012-2013 Messi ameichezea Barcelona mechi 50 katika mashindano yote.
No comments:
Post a Comment