Friday, June 14, 2013
SIMBA, YANGA RUKSA KWENDA SUDAN - SERIKALI.
HATIMAYE serikali imeziruhusu timu za Simba, Yanga na Falcon kwenda kushiriki mchuano ya Kombe la Kagame baada ya kupata barua kutoa serikali ya Sudan kwa timu hizo zitapewa ulinzi wa uhakika. Katika barua yake serikali ya Sudan iliihakikishia ile ya Tanzania kuwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa timu zote watakuwa salama katika kipindi chote cha mashindano hayo ya wiki mbili. Tayari timu za Simba na Yanga zilishatangaza kujitoa na kuvunja kambi walizoweka kwa ajili ya kujiwinda na mshindano hayo huku kukiwa na taarifa kuwa Baraza la Michezo kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA nao kuzialika timu zingine kuziba pengo hilo. Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla alithibitisha kupata barua kutoka Sudan ingawa hata hivyo alisisitiza kuwa timu za Simba, Yanga na Falcon wao ndio watakakuwa waamuzi wa mwisho wa kuamua kuzipeleka timu zao au la.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment