Saturday, June 15, 2013

PELE AKIPONDA KIKOSI CHA BRAZIL.

NGULI wa soka nchini Brazil, Pele amedai kuwa kikosi cha sasa cha timu ya taifa ya nchi hiyo hakiko imara kushinda Kombe la Shirikisho ambalo linaanza kutimu vumbi leo. Brazil ambayo kwasasa inaongozwa na kocha aliyeipa Kombe la Dunia 2002, Luiz Felipe Scolari wameonekana kutokuwa katika kiwango cha kuridhisha katika siku za karibu kitendo ambacho kimepelekea kutupwa mpaka katika nafasi ya 19 kwenye viwango vya ubora wa duniani. Na Pele amesema kikosi cha sasa hakiko vizuri pamoja na kuwemo kwa mshambuliaji nyota mpya wa Barcelona Neymar. Pele amesema pamoja na kwamba hafikirii kwamba Brazil itanyakuwa taji la michuano hiyo lakini huu utakuwa wakati mzuri kwa kocha na benchi lake la ufundi kutengeneza kikosi imara kwa ajili ya Kombe ya Dunia. Nguli huyo aliendelea kusema kuwa Brazil kwasasa ina tatizo la kukosa mawasiliano kati ya sehemu ya kiungo na ushambuliaji kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua katika mechi zao nyingi za kirafiki walizokuwa wakicheza.

No comments:

Post a Comment