Wednesday, June 19, 2013

PUYOL AFANYIWA UPASUAJI WA GOTI KWA MARA YA TATU.

BEKI mahiri wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia ambao utamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu mpaka nne. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mtandao wa klabu hiyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo leo. Puyol mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara katika miaka ya karibuni ukiwemo upasuaji wa mguu huohuo mara mbili, kuvunjika mfupa wa taya na pia kuteuka kiwiko cha mkono wake. Majeraha hayo yalimlazimu nyota huyo kukosa michuano ya Euro 2012 ambapo Hispania walitawadhwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo na pia kuenguliwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichopo nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment