Wednesday, June 19, 2013
VENUS AJIONDOA WIMBLEDON.
MWANADADA nyota katika mchezo wa tenisi, Venus Williams amelazimika kujiondoa katika michuano ya Wimbledon ambayo inatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo kutokana na matatizo ya mgongo. Williams mwenye umri wa miaka 33, amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo wakati wa michuano huo kwenye viwanja vya udongo na hajacheza toka alipojitoa katika michuano ya wazi ya Ufaransa iliyomalizika mapema mwezi huu. Mwanadada huyo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kuthibitisha kutoshiriki kwake kwenye michuano hiyo ili kuongeza muda ili majeraha yanayomsumbua yaweze kupona vyema. Williams ambaye amewahi kushika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake amewahi kushinda taji la mchezaji mmoja mmoja wa mashindano hayo mwaka 2000, 2001, 2005, 2007 na 2008.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment