Tuesday, June 18, 2013

RIBERY, BENZEMA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.

WACHEZAJI wawili wa kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery na Karim Benzema wamefikishwa mahakamani leo jijini Paris wakituhumiwa kutembea na mwanamke anayejiuza mwenye umri mdogo. Ribery ambaye anacheza katika klabu ya Bayern Munich na Benzema anayekipiga katika klabu ya Real Madrid watakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini inayozidi euro 45,000 kama wakikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo. Nyota hao wote wawili walikana tuhuma hizo huku mwanamke huyo aitwaye Zahia Dehar alitoa ushahidi kuwa wote wawili hawakuwa wakijua kama hajafikisha umri huo wakati wakifanya naye mapenzi mwaka 2008 na 2009. Pamoja na kwamba umri halali ni miaka 15 nchini Ufaransa lakini kumlipa mwanamke anayejiuza chini ya umri wa miaka 18 ni kosa.

No comments:

Post a Comment