KLABU ya Al Ahly ya Misri imeliomba Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kusogeza mbele mchezo wao dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini mpaka Agosti 9 mwaka huu. Mkurugenzi wa michezo wa Al Ahly Sayed Abdul Hafez alithibitisha timu hiyo kuandika barua rasmi kwa CAF ya kusogeza mbele mchezo huo mpaka Agosti 9 badala ya Agosti kama ulivyopangwa kwasababu ya mfungo wa mwezi wa Ranadhan ambapo wacheza wengi wa timu hiyo wanakuwa wamefunga. Hafez pia aliongeza kuwa Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi hiyo imekataa kuwawekea ulinzi kwa ajili ya mchezo huo jijini Cairo au Alexandria hivyo wanatarajia mechi hiyo kuchezwa katika mji wa El Gouna au Aswan. Hafez amesema wamefikia hatua hiyo baada ya timu hiyo kucheza dhidi ya Zamalek mchana na wachezaji kukataa kufungulia ambapo wote waliathirika mpaka hivi sasa kutokana na kucheza kwenye jua kali huku wakiwa wamefunga. Naye kocha wa Pirates Roger De Sa ameonyesha wasiwasi wake wa kucheza na Al Ahly jijini Cairo kutokana na vurugu zinazoendelea lakini anaamini kuwa CAF itatoa uamuzi sahihi kuhusiana na mahali patakapochezwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment