MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar amekabidhiwa tuzo ya mpira wa dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho. Mshambuliaji huyo alifunga mabao manne katika mechi tano za michuano hiyo alizocheza likiwemo bao katika mchezo wa fainali dhidi ya Hispania iliyochezwa alfajiri ya kuamkia leo kwa huku kwetu ambapo Brazil walitawadhwa mabingwa wapya wa kombe hilo kwa kuibugiza Hispania kwa mabao 3-0. Kiungo mahiri wa Hispania Andres Iniesta alitunukiwa mpira wa fedha kama mshindi wa pili na kiungo wa Brazil Poulinho alitunukiwa mpira wa shaba kama mshindi wa tatu.
Mshambuliaji wa Hispania Fernando Torres aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo na kukabidhiwa kiatu cha dhahabu kwa kufunga mabao matano, mshindi alikuwa mshambuliaji wa Brazil Fred aliyefunga mabao matano pia lakini walipishana muda wa kufunga mabao hayo na kupewa kiatu cha fedha na mshindi wa tatu ni Neymar aliyefunga mabao manne na kupewa kiatu cha shaba. Mbali na tuzo hizo pia golikipa wa Brazil Julio Cesar alishinda tuzo ya golikipa bora wa mashindano na kukabidhiwa glovu za dhahabu huku timu ya Hispania ikishinda tuzo ya Fair Play.
No comments:
Post a Comment