Monday, July 1, 2013
HAMILTON AITAKA PIRELLI KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUHUSIANA NA MAGURUDUMU YAO KABLA MADHARA MAKUBWA HAYAJATOKEA.
DEREVA nyota wa magari yaendayo kasi ya langalanga kutoka timu ya Marcedes, Lewis Hamilton amesema kampuni ya magurudumu ya Pirelli inatakiwa kuchukua hatua mapema baada ya magurudumu kuharibika vibaya katika mashindano ya British Grand Prix. Madereva wanne walipasukiwa na matairi katika mashindano hayo, huku Hamilton yeye akipasukiwa tairi lake katika mzunguko wa saba wakati akiongoza mbio hizo. Hamilton alitoa tahadhari kuwa hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa na Pirelli ili kuzuia matatizo kama hayo siku za usoni kwani inaweza kuwa hatari zaidi hata kufikia watu kupoteza maisha. Katika mbio hizo Hamilton alishika nafasi ya nne huku dereva mwenzake wa timu ya Marcedes Nico Rosberg akishinda mbio hizo na kufuatiwa na Mark Webber wa Red Bull wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Fernando Alonso wa Ferrari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment