Friday, July 12, 2013

FIFA YAFUATILIA KASHFA YA UPANGAJI MATOKEO NIGERIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA linafuatilia kwa karibu kuhusu kashfa ya upangaji matokeo inayozikabili vilabu viwili vya soka vya ridhaa nchini Nigeria iliyotokea wiki iliyopita. Katika matokeo ambayo yanaonekana kama ya mchezo wa kriketi, klabu ya Plateau United Feeders iliibugiza Akurba FC kwa mabao 79-0 wakati Police Machine wao waliitandika Bubayaro FC kwa mabao 67-0 mwishoni mwa wiki iliyopita. Hatua uchunguzi kwa vilabu hivyo imekuja kutokana na timu hizo kuhitaji matokeo ya aina hiyo ili waweze kupanda daraja. Ambapo katika taarifa yake FIFA imedai kuwa inafuatilia tukio hilo la tmu hizo za Nigeria kwa karibu ili kuona jinsi gani Shirikisho la Soka la nchi hiyo, NFF litatatua tatizo hilo. FIFA inafanya hivyo kwa kutambua kuwa suala hilo ni la ndani hivyo NFF ina wajibu wa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahiki kama ikigundulika aina yoyote ya udanganyifu katika mechi hizo.

No comments:

Post a Comment