
Monday, July 15, 2013
MAICON HANA NAFASI KATIKA KIKOSI CHANGU - PELLEGRINI.
MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa beki mahiri wa klabu hiyo Maicon ataondoka katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil alisajiliwa na City kutokea Inter Milan ya Italia kwa uhamisho wenye thamani ya euro milioni nne mwaka mmoja uliopita lakini ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza toka atue hapo. Wakati kukiwa na tetesi kuwa Maicon anapanga kujiunga na AS Roma ya Italia, Pellegrini ambaye ni raia wa Chile alibainisha kuwa beki huyo hayuko katika mipango yake ya msimu ujao hivyo lazima ataondoka. Pellegrini amesema kwasasa hawana haraka ya kuleta wachezaji wapya lakini wanahitaji wachezaji wawili au watatu zaidi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ili kujiimarisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment