Saturday, July 20, 2013

TERRY ASIPOJITUMA HAYUKO SALAMA CHELSEA - MOURINHO.

MENEJA mpya wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza kuwa nahodha wa klabu hiyo John Terry anatakiwa kujituma zaidi ili kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza na pia kupewa mkataba mpya. Terry mwenye umri wa miaka 32 ndio alikuwa nahodha katika kipindi cha mwaka 2004 hadi 2007 wakati Mourinho akiinoa klabu hiyo kwa mara ya kwanza ambapo umebakia mwaka mmoja kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika. Akihojiwa Mourinho amesema Terry anajua kuwa hayuko salama kitu pekee ambacho anajua kiko salama ni urafiki wao lakini linapokuja suala la kazi hakuna aliyekuwa salama. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anajua kuwa Terry ni mchezaji mzuri lakini anakiwa kuonyesha kiwango chake kama ilivyo kwa wachezaji wengine wote wa kikosi chake. Mourinho pia amedai kuwa na uhakika wa kumuibua tena mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Fernando Torres ambaye amekuwa akicheza chini ya kiwango toka awasili Stamford Bridge Januari mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment