Sunday, July 21, 2013
VILANOVA AANDIKA BARUA YA WAZI KUISHUKURU KLABU, MASHABIKI NA WOTE WENYE KUMTAKIA AFYA NJEMA.
MENEJA wa zamani wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova ameandika barua ya wazi kuishukuru klabu, mashabiki na wale wote wanaomuombea apone haraka baada ya kutangaza kujiuzulu rasmi Ijumaa iliyopita kwasababu ya maradhi ya saratani yanayomsumbua. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji wa kuondoka uvimbe wa saratani katika koo Nevemba mwaka 2011 na baadaye Desemba mwaka jana kufanyiwa upasuaji mwingine baada ya uvimbe kujirudia na kisha kufanyiwa matibabu ya mionzi kwa wiki 10 jijini New York mapema mwaka huu. Vilanova alirejea katika benchi la ufundi la Barcelona Machi mwaka huu na kuingoza klabu hiyo kushinda taji la Ligi Kuu nchini Hispania lakini aliachia ngazi Ijumaa kwasababu ya kuhitajika kuendelea na matibabu zaidi. Katika barua yake Vilanova amesema miaka mitano ambayo amefanya kazi na klabu hiyo toka akiwa msaidizi wa Pep Guardiola ilikuwa ni ya furaha kwake kwani imetimiza ndoto zake ambazo kocha yoyote angependa kupitia katika maisha yake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa matibabu ambayo anatakiwa kupewa kuanzia hivi sasa imeshauriwa na madaktari kuwa hawezi kutimiza majukumu yake kwa silimia 100 ya kukinoa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ndio maana ameamua kuachia ngazi. Vilanova aliwashukuru wachezaji, viongozi na madaktari wa timu hiyo kwa ushiriano waliompa kwa kipindi chote ambacho amekuwa nao toka alipogundulika kuwa na saratani miaka miwili iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment