JUMLA ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Kwa upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne Nyamlani,Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace Karia. Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii. Ahmed Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe Kiteve, James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge. Athuman Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Ernest Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed. Wengine ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao. Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee. Kwa upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti). Walioomba nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
No comments:
Post a Comment