Wednesday, August 7, 2013

ALVES ACHUKIZWA NA HATUA YA BARCELONA KUMUACHA ABIDAL.

BEKI mahiri wa klabu ya Barcelona, Dani Alves ameonyesha kuchukizwa na jinsi klabu hiyo ilivyomtenda Eric Abidal ambaye aliachwa katika kikosi cha timu hiyo katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Abidal mwenye umri wa miaka 33 ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Monaco ya Ufaransa alipambana na kurejea tena uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine baada ya kugundulika kuwa na uvimbe wa saratani April mwaka jana. Alves amesema kuondoka kwa Abidal kulimshangaza haswa ukizingatia kipindi kigumu alichopitia hivyo angependa aendelee kuwepo kutokana na juhudi alizozionyesha kukabiliana na changamoto zilizomkabili. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil amesema angejisikia vyema kama klabu hiyo ingemuongeza mkataba Abidal ili kuonyesha mfano ni kiasi gani wanajali.

No comments:

Post a Comment