BEKI mahiri wa kimataifa wa Brazil amemkingia kifua mchezaji mwenzake wan chi hiyo na klabu ya Barcelona, Neymar kwa kuamua kutokwenda katika mkutano wa wanahabari kabla ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Switzerland. Mshambuliaji huyo nyota mwenye umri wa miaka 21 alikuwa amepangwa kuzungumza katika mkutano na wanahabari jijini Basel lakini aliamua kuahirisha dakika za mwisho na kuzua hasira kwa wanahabari waliohudhuria. Badala yake Dani Alves alihudhuria kutano huo na kuwaomba wanahabari kuwa kupunguza hasira na kujaribu kumuelewa nyota huyo ambaye katika kipindi cha karibuni amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa anaemia ambao humsababishia uchovu. Alves amesema kila mtu amekuwa akizungumzia tatizo hilo linalomkabili katika kipindi cha hivi karibuni hivyo ni muhimu kwake kujaribu kupumzika ili ili aweze kurejea kurejea katika hali yake ya kawaida.
No comments:
Post a Comment