KAMATI ya rufani ya Shirikisho la Soka nchini Ufaransa-FFF imeondoa adhabu ya kuikata alama mbili klabu ya Monaco lakini imeshikilia uamuzi wa timu hiyo kucheza mechi moja milango ikiwa imefungwa. FFF imedai kuondoa adhabu hiyo ya kuikata Monaco alama mbili waliyopata baada ya mchezo wao wa Ligue 2 dhidi ya Le Mans Mei 17 wakati mashabiki wao walipowasha mafataki na kuvamiwa uwanjani. Mshabiki mmoja pia alimvamia mwamuzi katika tukio hilo ambalo lilitokea baada ya Monaco kufanikiwa kurejea katika Ligi Kuu nchini maarufu kama Ligue 1. Monaco ilicheza mchezo wake wa ufunguzi wa Ligue 1 Jumamosi iliyopita dhidi ya Bordeaux ambao walishinda kwa mabao 2-0. Mbapo watatakiwa kucheza milango ikiwa imefungwa katika mechi yao ya JUmapili ijayo dhidi ya Montpellier.
No comments:
Post a Comment