KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri ameomba radhi kwa tabia yake lakini amesisitiza kuwa hajaua mtu hivyo anapaswa kupewa nafasi nyingine ya kujirekebisha. Kiungo huyo anayecheza katika klabu ya Manchester City alifungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka la Ufaransa kufuatia kumtukana mwandishi katika michuano ya Ulaya 2012 na hajaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo toka kipindi hiko. Hatahivyo Nasri sasa yuko tayari kurejea katika mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Ubelgiji baada ya kocha Didier Deschamps kuridhishwa na tabia ya mchezaji huyo. Nasri mwenye umri wa miaka 26 aliomba radhi kwa tukio alilofanya katika michuano hiyo mwaka jana na kudai kuwa angetakiwa kukabiliana na tatizo hilo kwa weledi zaidi kuliko alivyofanya. Nyota aliendelea kudai kuwa anashukuru kupewa nafasi nyingine ya kujirekebisha na ana mategemeo yaliyotokea hayatajirudia kwasababu hivi sasa anajua jinsi gani ya kumudu hasira zake tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
No comments:
Post a Comment