KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Brazil, Luiz Gustavo anatarajiwa kukubali uhamisho wake kwenda Arsenal ili aweze kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil. Kiungo huyo mkabaji wa Bayern Munich ambaye amejikuta akishindwa kupata namba ya moja kwa moja katika kikosi cha kwanza anakaribia kukamilisha usajili wake wa paundi milioni 14 kwenda Emirates wiki hii. Gustavo anaamini kuwa nafasi yake itazidi kuwa finyu chini ya kocha mpya Pep Guardiola ambaye ameonyesha kumtumia sasa Javi Martinez ambaye naye anacheza nafasi hiyo ndio maana anaona uhamisho wake kwenda Arsenal unaweza kumsadia. Akihojiwa jijini Basel kabla ya mchezo wa kirafikiwa kimataifa baina ya Brazil na Switzerland kesho, Gustavo amesema mkataba wake na Bayern unamalizika 2015 lakini ni muhimu kwake kucheza katika kikosi cha kwanza ili aweze kuitwa katika timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment