MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kwa upande wa wanawake, Murielle Ahoure kutoka Ivory Coast amefanikiwa kuweka historia katika mbio za mita 100 kwa kuwa mwanamke wa kwanza wa Afrika kushinda medali ya dhahabu katika michuano ya riadha ya dunia inayoendelea jijini Moscow, Urusi. Ahoure mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni binti wa generali Mathias Doue aliyekuwa mmoja wa maofisa wa juu katika jeshi la Ivory Coast mpaka alipoondolewa na rais wa zamani wan chi hiyo Laurent Gbagbo mwaka 2004, amepania kuandika upya historia katika michuano hiyo kwa kuongeza medali nyingine ya dhahabu katika mbio za kita 200. Mbio za kufuzu kwa ajili ya fainali itakayofanyika Ijumaa zinatarajiwa kuanza Alhamisi. Ahoure ambaye pia alifika fainali yam bio za mita 100 na 200 katika michuano ya olimpiki mwaka jana alipambana vilivyo na kumwangusha bingwa mtetezi wa mbio hizo Carmelita Jeter aliyeshika nafasi ya tatu. Malengo makubwa ya Ahoure ambaye ametumia muda mwingi wa maisha yake katika nchi za Ulaya na Amerika amesema kuwa anataka kuwa mfano kwa wanariadha wa Afrika na kuwakataza kwenda nchi zingine kukubali kulipwa hela kwa ajili ya kubadilisha uraia na kukimbia kwa ajili yao mfano mzuri ikiwa nchi ya Qatar ambayo huwalipa wanariadha wa Kenya na Ethiopia kwa ajili ya kubadili uraia.
No comments:
Post a Comment