MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Liverpool, Luis Suarez amebadili mawazo kuhusu mustakabali wake na kusisitiza kuwa ameamua kubakia Anfield. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amekuwa akitaka kuondoka Uingereza kutokana na kuchoshwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo lakini Liverpool walikuwa hawako tayari kumuachia nyota huyo. Arsenal ambao ushiriki wao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ulionyesha kumvutia Suarez, walijitahidi kujaribu kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa kutoa ofa ya paundi milioni 42 ambayo ingevunja rekodi yao ya usajili lakini walikataliwa. Akihojiwa jijini Tokyo akiwa katika majukumu ya timu yake ya taifa, Suarez amebainisha kuwa ameamua kubakia kwa ajili ya mashabiki wa klabu hiyo ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwake.
No comments:
Post a Comment