MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Michezo-CAS imetupilia mbali rufani ya klabu ya Fenerbahce ya kufungiwa miaka miwili na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kwa kosa la kupanga matokeo. Katika taarifa yake CAS ilidai wameamua kutupilia mbali rufani hiyo kwa kukosa ushahidi hivyo adhabu waliyopewa na UEFA itaendelea kama kawaida. Kwa taarifa hiyo Fenerbahce ambao ilikuwa washiriki michuano ya Europa League msimu huu baada ya kuenguliwa na Arsenal katika mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa wataondolewa katika ratiba ya michuano hiyo ambayo inatarajiwa kupangwa Agosti 30. Fenerbahce walifungiwa na UEFA Juni mwaka huu baada ya maofisa wake kusaidia kupanga matokeo na kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uturuki mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment