KLABU ya Inter Milan ya Italia imetangaza kuongeza mkataba wa udhamini na kampuni ya Nike kwa miaka 10 zaidi na kupelekea ushirikiano na kampuni hiyo kufikia miaka 25. Mara ya kwanza Inter kuingia ubia na kampuni hiyo ya Marekani ilikuwa ni mwaka 1998, ambapo Nike bado inafaidi mikataba kama hiyo na vilabu vingine vikubwa duniani kama Manchester United na Barcelona. Pamoja na Inter kushindwa kufanya vizuri msimu uliopita ambapo walimaliza katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia, mkataba huo utawasaidia kujiimarisha ili kurejesha makali yao kama ilivyokuwa zamani. Inter ambayo kwasasa inanolewa na kocha mpya Walter Mazzarri, ilianza msimu mpya wa ligi kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Genoa Jumapili iliyopita.
No comments:
Post a Comment