KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe Scolari ametabiri kuwa nyota wa Barcelona Lionel Messi ataendelea kuwa mchezaji bora duniani kwa kipindi cha miaka mingine miwili zaidi. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina ameshinda tuzo nne mfululizo za Ballon d’Or na Scolari bado anaamini kuna vitu vingi vinakuja kutoka kwa nyota huyo mwenye miaka 26 kabla ya umri haujaanza kutafuna kiwango chake. Scolari pia alimsifu mchezaji huyo kwa kuwa na kipaji cha hali ya juu na uwezo mkubwa wa kubadili mchezo mwenyewe pindi timu yake inapozidiwa. Mbali na Messi, Scolari pia alimnadi mshambuliaji mpya wa Barcelona Neymar kuwa naye atakuja kung’ara kama ilivyo kwa Messi katika kipindi kifupi kijacho. Scolari amesema msimu huu utakuwa muhimu kwa Neymar kwa ajili ya kusoma na kuyazoea mazingira mapya ya Ulaya lakini hana shaka kwamba atachukua kipindi kifupi kuzoea hali hilo na kufanya maajabu kama ilivyokuwa Brazil.
No comments:
Post a Comment