MCHEZAJI nyota wa tenisi kutoka Uingereza Andy Murray amekiri kuwa hana uhakika kama ataweza kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Marekani au US Open lakini anategemea kuwepo kwake katika michuano ya Cincinnati kutampa maandalizi mazuri. Murray ambaye alimaliza ukame wa miaka 77 wa nchi yake kusubiria taji la Wimbledon mwezi uliopita amesema pamoja na na kushinda mataji mawili ya Grand Slams bado anaona anakabiliwa na changamoto mpya ya kutetea taji lake la US Open. Murray anayeshika namba mbili kwa ubora amesema changamoto kubwa inatoka kwake mwenyewe ya jinsi gani atavyocheza katika michuano hiyo huku akitegemea kucheza kwa kiwango cha juu kama ilivyokuwa katika michuano Wimbledon. Michuano ya US Open inatarajiwa kuanza kutimua Agosti 26 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment