MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amedai kuwa kila kitu kimetatuliwa kuhusiana na mustakabali wa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Luis Suarez. Arsenal wamekuwa wakimnyatia nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay kwa muda mrefu toka dirisha la usajili la majira ya kiangazi lilipofunguliwa lakini wameonekana kukaa kimya toka ofa yao ya paundi milioni 40 ilipokataliwa na Liverpool. Akihojiwa mara baada ya ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata timu yake dhidi ya Stoke City, Rodgers alidai kuridhishwa na mambo yanavyokwenda juu ya sakata la Suarez na ana mategemeo wanaweza kuendelea na mambo mengine katika kipindi kifupi kijacho. Rodgers amesema Suarez bado ni sehemu ya kikosi chake na amewapongeza mashabiki wa klabu hiyo kwa kumuunga mkono yeye pamoja na wachezaji wake.
No comments:
Post a Comment