MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya kipigo cha mabao 3-1 nyumbani kutoka kwa Aston Villa katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Mashabiki walikuwa wakikizomea kikosi cha Wenger huku wakipiga kelele kumtaka Mfaransa huyo kusajili wachezaji wengine ili kuimarisha timu hiyo kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi halijafungwa Septemba 2. Wenger amesema anachukizwa na kitendo cha kuwaudhi mashabiki ambao wanaipenda klabu hiyo hivyo anawaomba radhi kwa matokeo ambayo hawakuyategemea. Kocha huyo ambaye mpaka sasa amemsajili mshambuliaji mmoja pekee Yaya Sanogo amesema kwasasa inabidi wasahau mchezo huo na kuhamishia mawazo yao katika mchezo wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Fernebahce na kuhakikisha wanatapata matokeo mazuri.
No comments:
Post a Comment