KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amedai kuwa nchi zitakazoomba kuandaa michuano ya Kombe la Dunia miaka ijayo zitatakiwa kwanza zipate kibali kutoka katika mabunge yao. Kauli hiyo ya Valcke imekuja kufuatia misuguano iliyojitokeza kati ya FIFA na serikali ya Brazil kuhusiana na maandalizi ya michuano hiyo mwakani. Valcke amesema wanatakiwa kujifunza kitu fulani kutokana na matatizo waliyopata nchini Brazil ndio maana ameona kuna haja ya nchi kupata ridhaa ya mabunge yao kwanza kabla ya kutafuta nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano hiyo. Serikali ya Brazil na FIFA zimejikuta katika msuguano katika mambo kadhaa ikiwemo suala la kuuza pombe viwanjani kitu ambacho kilifungiwa nchini humo lakini imebidi waruhusu kwasababu mojawapo ya wadhamini wa FIFA ni kampuni za pombe.
No comments:
Post a Comment