Saturday, September 21, 2013

ANCELOTTI ALINIBAKISHA MADRID.

WINGA mahiri wa klabu ya Real Madrid, Angel Di Maria amebainisha kuwa aliamua kubakia klabuni hapo baada ya kujadiliana mustakabali wake na muargentina mwenzake anayecheza klabu ya Paris Saint-Germain Ezequiel Lavezzi na kocha wake carlo Ancelotti. Kulikuwa na tetesi kuwa winga huyo alikuwa akitaka kuondoka Santiago Bernabeu mapema katika kipindi cha usajili wa majira wa kiangazi lakini alichagua kubakia pamoja na ugumu wa kupata namba katika kikosi cha Madrid kilichosheheni nyota kibao. Di Maria amesema aliamua kubakia pamoja na kujua aina ya wachezaji ambao wangekuja klabuni hapo kwasababu anajiamini kwa kipaji alichokuwa nacho. Nyota huyo anasema mbali na kuzungumza na Lavezzi lakini pia alizungumza na Ancelotti na alimuhakikishia kuwa mchezaji atakayekuwa bora ndio atakayempanga katika kikosi chake cha kwanza.

No comments:

Post a Comment