Saturday, September 21, 2013

FIFA YASHTUSHWA NA UVUNJIFU WA SHERIA KATIKA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA AFRIKA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limestushwa na jinsi timu za Afrika zilivyovunja sheria kwa kuchezesha wachezaji wasioruhusiwa katika mechi zake za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Mechi nane katika kinyang’anyiro hicho zilikumbwa na matatizo hayo kwasababu timu mojawapo ilichezesha mchezaji ambaye uraia wake una utata au yuko katik adhabu. Katika kesi zote hizo baadhi ya timu zilijikuta zikipewa ushindi wa mabao 3-0 baada ya wapinzani wao kukutwa na hatia hivyo kuathiri msimamo wa makundi kwa kiasi kikubwa. Katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF, Mustapha Fahmy amesema kuna haja ya kulifanyia kazi suala hilo ili kujua kiini cha matatizo hayo na kujaribu kuzia yasije tokea tena siku za usoni. Mojawapo ya kesi za hivi karibuni ni Cape Verde kukosa nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ili kupata timu tano za Afrika zitakazokwenda Brazil mwakani kwa kumchezesha mchezaji aliyekuwa kwenye adhabu katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Tunisia.

No comments:

Post a Comment