Saturday, September 21, 2013

MAN UNITED, CITY KUONYESHANA KAZI.

KLABU mahasimu kutoka mji mmoja za Manchester United na Manchester City zitajitupa uwanjani kukwaana kwa mara ya 166 huku kila mmoja akijua kipigo kitamuweka katika hatari ya kukaa mbali katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchi Uingereza. Katika msimu huu ni mechi pekee zimeshachezwa na kila timu mpaka sasa lakini timu zote hizo tayari zimeshapoteza alama ambapo United ilitoa sare na Chelsea na baadae kupoteza mchezo dhidi ya Liverpool huku City wao wakitoa sare na Stoke City na kupata kipigo kutoka kwa Cardiff City. Timu zote mbili ziko nyuma ya vinara wa ligi hiyo Liverpool kwa alama tatu na kama timu yoyote ikifungwa kwenye mchezo huo itajikuta ikiwa nyuma kwa alama sita hatua ambayo itawawia vigumu kupanda tena. Makocha wa timu zote mbili David Moyes wa United na Manuel Pellegrini wa City hiyo itakuwa mechi yao ya kwanza kukutana lakini Moyes ndio anayepewa nafasi kubwa kwasababu alikuwa na rekodi nzuri ya kuifunga City wakati akiinoa Everton. Katika misimu sita aliyokuwa meneja wa Everton, Moyes ameshinda mechi tisa kati ya 12 ambazo alikutana na City.

No comments:

Post a Comment