Saturday, September 21, 2013

TOTTI AONGEZA MIAKA MIWILI ROMA.

KLABU ya AS Roma ya Italia imethibitisha kuwa nyota wake Francesco Totti amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utanfanya kubakia Stadio Olimpico mpaka 2016. Mkataba wa sasa wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kina na viongozi wa klabu hiyo nguli huyo alibainisha kuwa ameamua kubakia. Akizungumza na waandishi wa habari Totti amesema amefurahi kupata miaka mingine miwili na ana uhakika itakuwa yenye mafanikio huku pia akimshukuru rais wa klabu hiyo James Pallota na watu wote waliofanikisha. Totti alitangaza kustaafu majukumu ya kimataifa baada ya Italia kushinda Kombe la Dunia 2006 lakini kiwango kikubwa alichoonyesha msimu uliopita ambapo alifunga mabao 12 katika mechi 36 za Serie A, kimezua tetesi kuwa anaweza kurejea katika kikosi cha timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment