Saturday, September 21, 2013

UINGEREZA, SCOTLAND, WALES NA JAMHURI YA IRELAND KUTAFUTA UENYEJI EURO 2020.

SHIRIKISHO LA Soka barani Ulaya-UEFA limedai kuwa nchi za Uingereza, Scotland, Wales na Jamhuri ya Ireland ni mojawapo ya nchi zilizotuma maombi ya kuandaa mechi za michuano ya Ulaya 2020. UEFA imesema jumla ya nchi 32 ambao ni wanachama wake zimeonyesha nia ya kuandaa michuano hiyo baada ya maamuzi ya kufanya mashindano kuchezwa katika miji 13 kuzunguka bara la Ulaya. Uingereza inataka kuandaa mechi zake jijini London, Scotland imechagua Glasgow, Wales wamechagua mji wa Cardiff wakati Jamhuri ya Ireland wao watatumia mji wa Dublin. Mbali na hao lakini pia nchi vigogo wa soka barani humo wakiwemo Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uholanzi na Hispania pia na zenyewe zimeonyesha nia ya kutaka kuandaa mechi za michuano hiyo. UEFA itatoa uamuzi Septemba 25 mwakani nchi 13 ambazo zitakuwa wenyeji wa michuano hiyo. 


No comments:

Post a Comment